东非的年轻人,在听什么歌?
Bongo Fleva音乐(或称Bongo Flava),被看作是“东非大陆的Hip-Hop音乐”,自二十世纪八十年代开始在坦桑尼亚盛行。“Bongo”源自斯瓦希里语单词“ubongo”,意为“头脑、智力”,“Fleva”是英语“flavour”的谐音,因此“Bongo Fleva”的表层含义是指运用智慧的风采。
从深层次来看,“Bongo”在俚语中也可以指代坦桑尼亚或其主要城市达累斯萨拉姆(Dar es Salaam),人们在大都市中谋生多有不易,如何在街头巷尾的打拼中运用智慧和经验安身立命是青年不得不面对的课题,因此“Bongo Fleva”想要传达的思想是“街头智慧是立足于坦桑尼亚都市不可或缺的一部分”。在这个概念内,Bongo Fleva音乐顺理成章地成为坦桑尼亚青年一代对现实生活的文化表述。
二十世纪八十年代,随着坦桑尼亚政治体制改革和市场化经济的发展,以Hip-Hop音乐为代表的美国文化元素涌入坦桑尼亚,并凭借日新月异的传播媒介进入大众视野,备受年轻人追捧。
起初,模仿Hip-Hop音乐进行演唱的坦桑尼亚歌手以经济条件较好、易接触到外来文化的都市青年为主。后来,得益于坦桑尼亚电台DJ、电台MC的推荐与各类娱乐场所的增多,Hip-Hop音乐得以在年轻人之间广为流传,越来越多的新生代音乐人开始发现斯瓦希里语创作的巨大潜力。但受限于录音设备短缺,音乐工业化体系不完善,系统化的Bongo Fleva制作直至2000年以后才在坦桑尼亚完全展开。与此同时,本土音乐元素,如塔拉勃乐(taarab)、斯瓦希里语爵士乐(soukous)、恩戈马舞曲(ngoma),与外来音乐元素,如雷鬼(reggae)、蓝调(R&B)、迪斯科(disco)和祖克(Zouk)等,也一并融入Bongo Fleva的音乐创作中。
经过不断变化,Bongo Fleva最终发展成为具有坦桑尼亚独特风格的音乐形式。这一类歌曲的歌词以斯瓦希里语为主,夹杂英语或其他部族语言,在东非地区风靡一时。
除娱乐大众外,Bongo Fleva音乐还具有教育民众、揭露社会现象的意义。
歌曲主题涵盖社会生活的方方面面,常见主题包括关注贫穷问题、艾滋病预防、官员腐败以及音乐人的个人经历等。例如,著名的Bongo Fleva音乐人杰·莫伊(Jay Moe)通过首张专辑《是的,妈妈》(Ndio Mama)表达对早逝母亲的敬意,桑·索洛(Thang Solo)用歌曲表现自己作为音乐家的人生起伏,雷文尼(Rayvanny)的《我们的家》(Kwetu)坦然向女友介绍自己家徒四壁的情况,展现最真实的自己等等。
同时,Bongo Fleva音乐为东非地区的青年人提供了一个表达自我、畅所欲言的平台,歌词的现实讽喻意义往往能引起社会各界的高度关注。例如《你还会爱我吗》(Utanipenda)这首歌曲描述了音乐人戴蒙德(Diamond Platnumz)想象自己在人生低谷期会经历的世态炎凉,对无法预料的明天提出思考:
我无法偿还债务只能卖掉资产
广播和电视已不再播放我的歌曲
只徒留一个经纪人的名字
就连童话故事也不需要我
曾经用甜美话语赞美我的粉丝
如今却成为在照片墙上攻击我的敌人
(Nimeshindwa Kulipa BiMA Nimeuza Madalee
Radio Nyimbo Wamezima Tv Ndio Hataree
Umeneja Umebaki Jina
Hanitaki Hata Talee
Oooh Wale Mashabiki Walionisifu Kwa Maneno Matamu
Leo Maadui Zangu Ni Mitusi Tu Kwa Instagram)
……
我所说的话都饱含真理
因为没有人知道明天会发生什么
计划一切的上帝将真相都藏了起来
你祈祷着,丈夫我不再会是街头笑柄
因为昨天的朋友会成为明天的敌人
(Ooh Ninayosema Yana Maana
Sababu Hakuna Anaejua Kesho
Anaepanga Ni Rabana Ila Ameificha Ni Confidential
Ukisali Omba Sana Mumeo Nisije Kuwa Kichekesho
Maana Rafiki Wa Jana Ndio Adui Mkubwa Wa Kesho)
Bongo Fleva音乐就像坦桑尼亚青年倾诉的窗口,悠扬的旋律中,希望、梦想、困境和挣扎不断交织缠绕,他们把自己鲜明的个性和强烈的渴望以流行音乐的形式铺陈在大众面前,掷地有声,意味深长。
Muziki wa Bongo Fleva (au Bongo Flava) unachukuliwa kama “Hip-Hop katika Bara la Afrika Mashariki”, nao umeshamiri huko Tanzania tangu miaka ya themanini karne iliyopita. Neno “Bongo” linatokana na neno “Ubongo”, ambalo linamaanisha akili, na “Fleva” inatokana na matamshi ya neno lingine la Kiingereza “Flavour”. Kwa hiyo, fasili ya “Bongo Fleva” ni viburudisho vitokanavyo na matumizi ya akili. Zaidi ya hayo, Bongo inaashiria jiji la Dar es Salaam au Tanzania katika miktadha maalumu. Watu hukabiriwa na matatizo mengi wakati wanapoishi katika jiji kubwa. Kufuatana na hali zao ngumu, vijana wanapaswa kujifunza jinsi wanavyotumia busara na maarifa ya mtaani ili waendelee na maisha yao. Kwa hiyo, fasili ya pili ya Bongo Fleva ni kuwa ukitaka kuishi katika jiji la Tanzania, ni lazima uwe na busara hata ujanja .Kwa mujibu wa ufafanuzi huo, kizazi kipya kinaanza kujieleza kwa utamaduni maisha yao ya halisi huko Tanzania kwa njia ya muziki wa Bongo Fleva.
Wakati wa miaka ya themanini karne iliyopita, kufuatana na mageuzi ya kisiasa ya Tanzania na maendeleo ya mfumo wa soko huria, Sanaa za Kimarekani kama vile muziki wa Hip-Hop, graffiti mitaani na sanaa nyinginezo ziliingizwa Tanzania, nazo zilikaribishwa na kupendwa na hadhira, hasa vijana, kwa njia mpya ya vyombo vya habari. Mwanzoni, waimbaji wa Tanzania waliigiza muziki wa Hip-Hop na kutunga nyimbo, wengi wao walikuwa vijana wa tabaka la katikati ambao waliweza kugusa tamaduni za kigeni kwa rahisi.Baadaye, muziki wa Hip-Hop ulishamiri hadi kufikia vijana wote kwa sababu ya mapendekezo ya DJ na MC wa redio na kuongozeka kwa mahali pa kuburudishia. Pamoja na maendeleo hayo, wanamuziki wengi wapya waligundua uwezo mkubwa wa utungaji wa Kiswahili. Lakini kwa sababu ya ukosefu wa vifaa vya rekodi na mfumo rasmi wa utungaji wa muziki, Bongo Fleva ilikuza kwa upole hadi mwaka wa 2000. Wakati huo huo, elementi nyingi za muziki wa kienyeji, kama vile taarab, soukous na ngoma, ziliunganishwa na elementi za kigeni, kama reggae, R&B, disco na Zouk, majaribio haya yalipata mafanikio makubwa katika utungaji wa Bongo Fleva. Kisha Bongo Fleva ilikuwa muziki mwenye mtindo wa kipekee wa Tanzania pamoja na michango ya wanamuziki wengi maarufu. Nyimbo za Bongo Fleva ambazo ziliandikwa kwa Kiswahili na pia kuchanganywa na Kiingeraza au lugha zingine za kikabila, zilipendekeza sana huko Afrika Mashariki.
Zaidi ya kuwaburudisha watu, Bongo Fleva inaweza kuwafunza wananchi na kudhihirisha matatizo ya kijamii vilevile. Maudhui ya nyimbo hizi hugusa kila upande wa maisha ya kijamii, kama vile umaskini, kujikinga na UKIMWI, ufisadi, hata maisha ya wanamuziki wenyewe. Kwa mfano, mwanamuziki maarufu Jay Moe alitunga wimbo wake maarufu Ndio Mama kwa ajili ya kutoa heshima kwa hayati mama yake. Thang Solo alionyesha hali tete ya maisha yake katika nyimbo zake. Na Kwetu ni wimbo ambao Rayvanny alimjulisha mpenzi wake hali ngumu ya familia yake na kumwelezea hisia zake halisi.
Aidha, Bongo Fleva inawatolea vijana wa Afrika Mashariki njia ya kusawiri mawazo huria. Maneno yenye sitiari na kejeli yanayotumiwa katika nyimbo hizo huwavutia watu wa kila aina. Kwa mfano, wimbo wa Utanipenda unasimulia jinsi mwanamuziki Diamond Platnumz anavyofikiria ugeugeu katika maisha yanayojawa na uchungu mkubwa wa kihisia, na pia anatoa wasiwasi juu ya maisha ya usoni:
Nimeshindwa Kulipa BiMA Nimeuza Madalee
Radio Nyimbo Wamezima Tv Ndio Hataree
Umeneja Umebaki Jina
Hanitaki Hata Talee
Oooh Wale Mashabiki Walionisifu Kwa Maneno Matamu
Leo Maadui Zangu Ni Mitusi Tu Kwa Instagram
……
Ooh Ninayosema Yana Maana
Sababu Hakuna Anaejua Kesho
Anaepanga Ni Rabana Ila Ameificha Ni Confidential
Ukisali Omba Sana Mumeo Nisije Kuwa Kichekesho
Maana Rafiki Wa Jana Ndio Adui Mkubwa Wa Kesho
Bongo Fleva ni chombo kinachotumiwa na vijana wa Tanzania kutuonyesha hisia zao. Muziki huu wenye upekee huchanganya matumaini, ndoto, taabu na juhudi zao. Wanaonyesha roho na matumaini yao hadharani kwa njia ya muziki unaopendeza. Hisia na tamko lao bila shaka vitawagusa wasikilizaji kwa kina.
参考文献 / Marejeleo
[1] Kadallah, R.T., 2017. Muziki wa Bongo Fleva na Changamoto za Kimaadili katika Jamii. Mulika: Toleo Maalumu la Muziki wa Kizazi Kipya, Vol. 29 & 30.
[2]Fergus Ainsworth (2020) Bongo Flava : Tanzania’s home grown Hip Hop. [THE BEST OF AFRICA] 27th March. Available from:
https://thebestofafrica.org/content/bongo-flava-tanzanias-home-grown-hip-hop [Accessed 11/10/20].
[3] Mahenge, E., 2011. Chimbuko la Muziki wa Hip hop ni Uasi au Sanaa za Maonesho. Mulika: Toleo Maalumu la Muziki wa Kizazi Kipya, Vol. 29 & 30.
[4] Suriano, M., 2011. Hip-hop and Bongo flavour music in contemporary Tanzania: youths' experiences, agency, aspirations and contradictions. Africa Development, 36, pp. 113-126.
本文外语版首发于
上海外国语大学
多语种外文网(斯瓦希里语)
点击“阅读原文”查看
策划|青年学研中心 学术部
撰稿|宋艺婷(斯瓦希里语专业2018级学生)
审核|马骏老师 宁艺老师
编辑|青年学研中心 学术部 韩烨
图片来源于网络